ROMANTIC n RELATIONSHIP.

ENTERTAINMENT. BONGO CARTOONs. LOVE STORYs. DAR 2 MOSH. LYRICKs.





 WEMA SEPETU


LOVE SMS (Ujumbe wa Mahaba)


CHAGUA SMS NZURI KATI YA ZIFUATAZO, KISHA MTUMIE MPENZI WAKO...





Maji hunitosha nisikiapo kiu, chakula hinitosha nisikiapo njaa, lakini wewe hunifaa kwa kila kitu!

*****

You are the twinkle of my eyes, the smile on my lips, the joy of my face,

without you, I am incomplete!

*****

Najua unanipenda mpenzi wangu, lakini urembo wako unaniweka roho juu, angalia usihadaike na walaghai, napenda mpenzi wangu! Mwaaaa…

*****

Last night I matched each star with a reason for loving you. I was doing great until I ran out of stars!

*****

Niseme nini ujue nakupenda? Nifanye nini ujue nakupenda? Nikuite jina gani ujue ni wewe peke yakon upo moyoni mwangu? Hakika hakuna ila moyo wangu ndio naosema kuwa nakupenda, niamini mpenzi!

*****

God is wise when he did not put a price tag on you darling. If he did, I won’t be able to afford to have a boyfriend as precious as you. I luv you!

*****

Najua una kazi nyingi mpenzi, lakini muda wa kula umefika, nenda ukale kwanza mpenzi wangu!

*****

Darling, if you are the second best girl for me, then who is the best? The answer is nobody, because you will always be the best girl for me!

*****

Hakuna atakayetutenganisha mpenzi wangu, ingawa wanafiki wanasema mengi, weka masikio yako pamba, achana nao wana vivu hao!

*****

My heart for you will never break. My smile for you will never fade. My love for you will never end. I love you!

*****

Kama nikiambiwa niweke rekodi ya watu muhimu katika maisha yangu duniani, kwenye tatu bora utakuwepo, kwanza wazazi wangu halafu wewe unafuatia, nakupenda dear!

*****

When you need someone to be there for you, I’d be just sitting right beside you!

*****

Usiku huu ni mrefu ajabu, kuna baridi kali kuliko maelezo, natamani ungekuwa pembeni yangu nipate joto lako!

Ingawa upo mbali nami, lakini amini kuwa nakupenda kwa mapenzi yangu yote, lala salama dear, mwaaaaa!

Kila ninapovuta hisia ya kuwa na wewe nachanganyikiwa, natumia mto pembeni yangu naufananisha na wewe, nakupenda mpenzi..!

                                              THANX......

                                                                        (c)2008

                                                                           Steve.  


 ********@@@@@@@@**********@@@@@@@@

Kukuambia anakupenda pekee hakutoshi ikiwa...


Mungu ni mwaminifu sana katika maisha yetu, hakuna ambaye anaweza kupingana na jambo hilo. Ni nani atakayeweza kusimama na kusema mafanikio aliyonayo yanatokana na nguvu zake mwenyewe?

Nani anaweza kusema kwa ujasiri kuwa mke mwema aliye naye ni kwa ujanja wake? Hakuna! Ni Mungu mwenyewe ndiye muongozaji wa kila kitu. Huo ndiyo ukweli na utabaki kuwa hivyo.

Sasa tugeukie katika mada yetu la leo. Kwamba mpenzi wako anapokuambia anakupenda, inatosha kweli kukuthibitishia kuwa anakupenda kwa dhati na uendelee kumuamini? Hapa kila mmoja anaweza kuwa na jibu lake, lakini kwa Wataalamu wa Saikolojia ya Mapenzi hawakubaliani na hoja hii. Kwanini? Kwa sababu neno nakupenda ni jepesi sana katika hali ya kawaida kutamkika, lakini lina maana kubwa sana linapokuja katika ulimwengu wa mapenzi ya dhati.


Wanasaikolojia ya Uhusiano wanaeleza kwamba neno hilo linaweza kuwa na maana ikiwa litalandana na matendo. Wengi wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu katika uhusiano. Wapenzi wao wamekuwa hawaeleweki kama wana mapenzi ya kweli au lah, kutokana na mambo wanayowafanyia lakini kwa wakati huo huo neno nakupenda limekuwa halikauki midomoni mwao.

Ni haki yao kuchanganyikiwa, lakini kuchanganyikiwa huko kunatokana na kutokujua mambo ya uhusiano vyema. Inawezekana wewe ukawa mmoja wa watu hao, hii ni nafasi yako mahusus kwa ajili ya kumfahamu mpenzi wako kama anakupenda au anakupotezea muda.

ANAKUPUUZA...

Hili ni tatizo kubwa katika uhusiano na hasa wanaonyanyaswa na hili ni wasichana. Wanaume wengi wa siku hizi ambao wana mapenzi ya ubabaishaji huwapuuza wenzi wao.

Kwanini ukubali uendelee kuitwa mpenzi na wakati huo huo anakupuuza? Bado utaendelea kumhesabia mtu huyo anakupenda huku anakupuuza? Kwa lipi hasa wakati hazingatii yale unayomuambia hata kama yana msingi kwa maisha yenu yajayo?

Mpenzi mwenye mapenzi ya kweli kwanza huzingatia mawazo ya mpenzi wake, hupima kila aambiwalo na kulifanyia kazi. Huwezi kumpuuza mtu ambaye unampenda hata siku moja. Hiki ni kipimo cha kuzingatia wakati unatafuta mpenzi wa kweli.

Kama mpenzi wako haonyeshi kuthamini umuambiayo, penzi lake litakuwa na mushkeli. Anayekupenda huwa makini kukusikiliza kwa kila kitu. Mwingine anaweza akawa anamshauri vizuri sana juu ya maisha lakini mwanaume huyo akawa hana ‘time’ kabisa naye. Huyo hana mapenzi ya kweli.!

...ANAHOFIA SIMU YAKE

Hapa kuna utata mkubwa! Wengi hujitetea kuwa simu ya mkononi ni kwa ajili ya mhusika tu, hapa kuna ukweli fulani lakini wengi walio katika uhusiano hutumia sababu hii kama nguzo ya kuendelea kufanya mambo yao yasiyofaa kwa kutumia simu zao. Hata hivyo Wanasaikolojia ya Mapenzi wanaunga mkono hoja hiyo, maana wakati mwingine unaweza ukachukua simu ya mpenzi wako ikasababisha mgogoro mkubwa.

Kumgundua msaliti ni rahisi sana, ukiona unaposhika simu yake anakuwa mkali, jua kuna kitu kinaendelea.Simu inapigwa halafu ghafla anatoka kwenda kupokelea nje, jiulize mara mbili. Lakini wakati mwingine ukiona simu yake inaita halafu jina linalotokeza kwenye simu yake lina utata ama limeandikwa kwa kifupi, anza kufikiria mara mbili.

Ukianza kuhisi tofauti kidogo juu ya simu yake, anza kumchunguza na mara nyingi akigundua unamchunguza kuliko umharibie mambo yake atakuwa tayari kuachana na wewe. Kukuambia anakupenda pekee hakutoshi kuonyesha anakupenda kwa kasoro hii.

*******************************************

JE, WEWE NI MTUMWA WA MAPENZI?


Kuishi kama mtumwa wa ni hatari na huweza kupunguza hata ufanisi wako wa kazi. Kwanza kabla hatujafika mbali, hebu tuangalie maana ya utumwa wa mapenzi.

MAANA YA UTUMWA WA MAPENZI!
Hii ina maana pana sana, lakini naweza kutoa moja kama mjumuisho wa yote! Utumwa wa mapenzi unaweza kutokea pale, utakapompenda mtu ambaye hana habari na wewe kabisa, yaani unajikuta ukioza juu yake, lakini anakuwa hana mapenzi na wewe kabisa.

Wakati mwingine unaweza ukamshawishi mtu huyo kwa vitu fulani, akakubali kuwa na wewe lakini sio kwa mapenzi ila kwa kuwa kuna kitu fulani atapata kutoka kwako.
Kama ukiruhusu utumwa wa mapenzi, maisha yako ya kawaida, yanaweza kuharibika na kukosa muelekeo! Uwezo wako wa kufikiria utakuwa mdogo ma hata wakati mwingine kupunguza ufanisi wako wa kazi.
Muda mwingi utautumia kufikiri kwanini fulani hakuipendi? Una kasoro gani n.k, kimsingi kama ukiruhusu utumwa wa mapenzi, mpangilio wa maisha yako unaweza kuharika na kukosa muelekeo kabisa.

UTAJUAJE KAMA WEWE NI MTUMWA?
Hili ni rahisi kutambua ingawa ni hatua mbaya sana katika maisha yako. Jambo la kwanza ni mabadiliko ya hisia za moyo wako, utajikuta ukimpenda mtu sana, ambaye hata time kabisa na wewe! Pamoja na kuwa anaonyesha kila dalili za kukuchukia lakini bado utahisi kumpenda na kumhitaji katika maisha yako.
Moyo wako huendele kuysisitiza kuwa huyo sio sahihi kwa maisha yako, lakini bado mtu huyo ataendelea kukuonyesha kila vibwanga vya kuchukiza. Sio jamboi la ajabu kuhiusi kufa kuliko kuendelea kuteseka kwa penzi la huyo ambaye haonyeshi kutambua thamani ya penzi lako.

UTUMWA WA MAPENZI
Kipengele hiki ni kama kiini cha mada hii, tunapozungumzia utumwa halisi wa mapenzi, ni pale ulipojitahidi kumshawishi mpenzi huyo, kwa kila njia ili nuweze kuwa naye! Inawezekana ulimshawishi kwa pesa na wakati mwingine, ndugu zake walimlazimisha kuishi na wewe, akaamua ingawa hakupenda.

Mnapokuwa mmeingia kwenye ndoa, hapo sasa ndipo utumwa hukamilika! Sio rahisi kutoka tena (hasa kwa Wakristo) lakini mume/mke huyo atakuonyesha kila aina ya vimbwanga kuthibitisha kuwa hana mapenzi na wewe.
Inawezekana ukahitaji haki yako ya ndoa lakini akawa mgumu kukupa, kwa sababu hakupendi! Alikuoa/olewa na wewe kwa sababu ya shinikizo na sio mapenzi, lakini kwa kuwa tayari unakuwa umeshazoeana naye inakuwa vigumu kumtoa moyoni mwako.
Wengi wao hufikikia hatua ya kuamua maamuzi ambayo sio sahihi, baadhi yao huchanganyikiwa na wengine huona bora kufa kuliko kufedheheka! Kimsingi utumwa wa mapenzi ni ugonjwa mbaya sana kisaikolojia.
CHUNGUZA MOYO WAKE
Hakika utumwa wa mapenzi ni ugonjwa mbaya sana, kimsingi usiruhusu kabisa kuwa mtumwa wa mapenzi. Hilo linawezekana kwa kumchunguza moyo wa huyo umpendaye. Katika hali ya kawaida, ni jambo gumu kidogo lakini iunawezekana.
Unaweza kuuchunguza moyo wake kwa kuangalia je, ni kweli naye anakupenda kama unavyompenda? Kuna wengine hushindwa kukuambia SIKUTAKI, lakini anaendelea kuwa na wewe, kukufanya chombo cha starehe na kukupotezea muda wako. Ni rahisi kumtambua.
Mwulize kwanini anakupenda? Akupe sababu hasa za mapenzi yake kwako, akikuambia anakupenda kwa sababu ya umbo au sura nzuri, tambua huyo sio mpenzi sahihi na huenda akakufikisha katika utumwa wa mapenzi. Anayekupenda, hukujibu kuwa, amekupenda kama ulivyo, anaamini wewe ni mhimnili wa maisha yake na maisha yake yatakuwa kamili akiwa wewe na sio kuzungumzia habari za ngono!
Mara nyingi ukimpigia simu, huchelewa kupokea kwa kisingizio cha kazi nyingi, ukimwandikia sms ndio kabisa hajibu! Yote hiyo ni kwa sababu hakupendi! Hana msisimko wowote na wewe.
Kwanza kama anakupenda, hata kwenye simu yake atakuwa amekuwekea mlio (Ring tone) tofauti na wengine, hivyo ukipiga lazima ajue ni wewe na hata kama ana kazi nyingi kiasi gani anapaswa kupokea, kwa kuwa wewe ni muhimu kwake!
KATAA KUWA MTUMWA
Ukiona niliyoanisha katika kipengele kilichopita, ujue kuwa hakupendi, sasa kama ndivyo, huna sababu ya kukubali kuwa mtumwa! Kataa kwa nguvu na ni bora ukajifunza jinsi ya kukabiliana na hali ya kuishi bila huyo uliyempenda, kuliko kuishi naye halafu akutese.
Vipo vitu vingi vitakavyokusaidia kuepukana na hali ya sononeko katika moyo wako na kuishi maisha yako peke, huku ukimsubiri aliye maalum kwa ajili yako! Kataa kabisa kuwa mtumwa maana maisha yako huweza kuharibika moja kwa moja.

************************************************


SPECIAL KWA PENDO..!!!